Jackson Kioko awatahadharisha maafisa wa afya wanaopuuza majukumu na kusababisha vifo vya wajawazito

Mkurugenzi wa huduma za matibabu Jackson Kioko amewatahadharisha maafisa wa afya ambao hupuuza majukumu yao na kusababisha vifo vya wanawake wajawazito. Ukosefu wa huduma maalum, kucheleweshwa kwa matibabu kwa wanawake na ujuzi duni wa kimatibabu vimetajwa kuwa baadhi ya changamoto za kiafya zilizosababisha idadi kubwa ya vifo vya kina mama wanawake wajawazito mwaka wa 2014 kulingana na ripoti hiyo. Ripoti hiyoilionyesha kuwa ni mwanamke mmoja pekee kati ya kumi aliyefariki akijifungua hospitalini mwaka 2014 akipokea matibabu maalumu kutoka kwa mtaalam, hali iliyohoji kuwepo kwa wataalam katika taasisi za kimatibabu. Kioko alikuwa akiongea wakati wa uzinduzi wa ripoti ya kitengo cha afya ya mama katika wizara ya afya, ambapo ilibainika kuwa wanawke wengi wajawazito hupoteza maisha yao kati ya saa kumi na moja jioni na saa mbili asubuhi,mwishoni mwa wiki na wakati wa likizo za umma kutokana na ukosefu wa wahudumu wa kutosha.

Takriban asili mia 51 ya vifo hivyo huripotiwa kwenye hospitali za kiwango cha level 4. Kioko alisema wizara ya afya inalenga kupunguza kwa asili mia 50 A�vifo vya wanawake wajawazito wakati wa kujifungua kutoka 362 kati ya wanawake 100,000. Afya ya wanawake wajawazito imejumuishwa katika ajenda nne kuu za serikali ya Jubilee. the jubilee administration.