Jack Wilshere Amfanya Baba Wa Mpenziwe kuwa Baunsa

KIUNGO mkorofi wa Arsenal, Jack Wilshere ameamua kumfanya baba ya demu wake kuwa baunsa wake wa kumlinda kila anapokuwa kwenye mituko yake ya usiku.

Mzee Michael Michael ni kinyozi wake Wilshere ambaye hushughulika na kumtengeneza nywele kwenye saloni yake.

Lakini hata zaidi kando na kuwa kinyozi wa Wilshere, mzee huyo ndiye baba wa demu ya Wilshere kichuna mrembo Andriani Michael ambaye amekuwa naye katika uhusiano kwa takriban miaka mitatu hivi.

Wilshere na baba mkwe wake wana uhusiano mzuri sana tena wa karibu kando na kuwa kinyozi wake, suala la kuwa na binti yake imechangia kuwaleta karibu na kuwafanya kuwa washakaji wa karibu sana.

Ukorofi

Sasa Wilshere anayefahamika kwa ukorofi wake nje ya uwanja hasa anapozuru viwanja vya burudani ambapo mara nyingi huishia kuzua fujo, ameamua kwamba atakuwa anaandamana na Michael kwenye mituko yake hiyo ya usiku ili kuhakikisha kwamba anamlinda na kumzuia kufanya vitendo va upuzi vinavyoweza kumsababishia madhara mabaya.

Wilshere amefikia uamuzi huo kufuatia tukio la Jumapili iliyopita alipooneakana akizungumza na maafisa wa polisi nje ya kilabu ikiwa ni baada yake kuzozana na makundi mawili tofauti ya wanaume waliokuwa wanatishia kumshushia kipigo.

kwa Hisani ya swahili hub