Israel yaanda Mazishi Ya Shimon Peres

Taifa la Israel linaandaa mipango ya mazishi ya mmoja wa viongozi wake shupavu Shimon Peres ambaye alikuwa waziri mkuu wa nchi hiyo mara mbili na kisha rais. Peres aliaga dunia mapema leo akiwa na umri wa miaka-93 kutokana na ugonjwa wa kiharusi baada ya kulazwa hospitalini kwa wiki mbili. Peres ametajwa kuwa kiongozi shupavu aliyejitolea maishani mwake kuwatumikia raia wa Israel. Alikuwa msitari wa mbele katika harakati za kupigania amani kati ya Israel na wapalestina. Mwaka-1994 alipokea tuzo ya amani ya Nobeli kutokana na wajibu wake wa kuendeleza mpango wa amani na wapalestina. Peres alikuwa mmoja wa viongozi wa kizazi kilicho-ashiria kubuniwa kwa taifa la Israel mwaka-1848. Rais Uhuru Kenyatta amemtaja Peres kuwa kuwa kiongozi mjasiri aliyezingatia ukweli. Alisema ameungana na familia ya Peres na raia wote wa israel wakati huu wa majonzi. Rais Kenyatta alisema alifahamishwa kuhusu harakati za amani za kiongozi huyo wakati wa ziara yake ya hivi majuzi nchini Israel.