ISIS Yauwa Wanajihadi Nane Nchini Uholanzi

Wanamgambo wa kiislamu wamewaua wanachama nane wa uholanzi wa kundi la jihad kwa kuwalaumuA� kujaribu kujitenga na kundi hilo na kuwaasi. Hali ya wasiwasi ilitanda huko Raqa katika muda wa mwezi mmoja uliopita kati ya wanachama 75 wa jihad nchini Uholanzi miongoni mwao wakiwemo wapiganaji ambao asili yao ni kutoka Morocco na majasusi wa kundi la kiislamu kutoka Iraq. Wanachama wengine watatu wa jihad nchini uholanzi walikamatwa na wanachama wa kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Iraqi waliowashutumu kwa kutoroka na mmoja wa watu waliokuwa wakizuiliwa kupigwa hadi kufa wakati wa kuhojiwa. Viongozi wa kundi la wanamgambo wa kiislamu huko Raqa walituma wajumbe kutatua mzozo huo na wanachama wa kundi la jihad kutoka uholanzi lakini wakawaua wapatanishi katika kulipiza kisasi. Viongozi wa kundi la wanamgambo wa kiislamu waliagiza kukamatwa kwa wanachama wa kundi hilo la jihad na kuwazuilia huko Tabaqa na Maadan huko Syria.Kulingana na duru za kijasusi nchini Uholanzi watuA� 200 kutoka Uholanzi wakiwemo wanawake 50 wamejiunga na kundi la wanamgambo wa kiislamu huko Syria na Iraq.