IPOA yatarajiwa kuwatuza maafisa wa polisi walioshamiri katika kazi zao

Halmashauri huru ya kutathmini utendakazi wa polisi-IPOA ikishirikiana na wadau wa humu nchini na wale wa kimataifa inatarajiwa kuwatuza maafisa wa polisi walioshamiri katika kazi zao. Waziri wa usalama wa taifa, Joseph Nkaiserry anatarajiwa kuongoza hafla hiyo inayolenga kuhamasisha maafisa wa polisi kuimarisha utenda kazi wao kwa umma. Balozi wa Marekani hapa nchini Robert Godec ni miongoni mwa wageni wanaotarajiwa kwenye hafla hiyo itakayoandaliwa katika hoteli jijini Nairobi. Sherehe hiyo pia itatoa fulsa kwa wananchi ambao ndio wanahudumiwa na maafisa wa polisi kutathmini maafisa hao na vituo vya polisi ambako wamehudumiwa. Tuzo hizo zimeorodheshwa katika viwango vya afisa bora zaidi wa kike, afisa bora zaidi wa kiume, kituo bora zaidi cha kuzuiliwa na kituo bora zaidi cha polisi kwa uadilifu wa utendakazi na usafi.A�