IPOA yatakiwa kuchunguza polisi waliotumia nguvu kupita kiasi

Kituo Cha Sheria kimeitaka halmashauri huru ya kutathmini utendakazi wa polisi-IPOA ichunguze na kuwawajibisha maafisa wa polisi waliotumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na waandamanaji kufuatia kutangazwa kwa rais Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanywa tarehe 8 mwezi huu. Mkurugenzi mkuu wa Kituo Cha Sheria, Gertrude Angote, alisema maafisa wa polisi walitumia risasi kukabiliana na waandamanaji katika mitaa ya Mathare, Kibra na Kawangware, jijini Nairobi pamoja na Kisumu, Homa Bay na Siaya, miongoni mwa maeneo mengine yaliyoathiriwa. Alisema hatua ya maafisa wa polisi ya kutumia nguvu kupita kiasi, haifai na kwamba ni kinyume cha sheria. Angote alisema habari kutoka maeneo hayo zinaonyesha kwamba miili ipatayo ishirini na minne ina majeraha akiwemo msichana wa umri wa miaka-10 aliyeuawa huko Mathare pamoja na mtoto wa miezi sita aliyeaga dunia siku ya jumanne kutokana na majeraha aliyopata baada ya kujeruhiwa na polisi. A�