IPOA Yataka Maafisa Kuwajibika Katika Matumizi Ya Bunduki

Halmashauri huru ya kutathmini utendakazi wa polisi (IPOA) imeitaka huduma ya taifa ya polisi kuwahamasisha maafisa kuhusu vifungu vya katiba na sheria ya huduma hiyo ya kukabiliana na utumiaji mbaya wa bunduki nguvu kupita kiasi. Kwenye taarifa kwa vituo vya habari, halmashauriA� hiyo imewahimiza maafisa wakuu wa polisi kujifunza kutokana na mauaji yaA� Kwekwe Mwandaza mwenye umri wa miaka 14 yaliyotekelezwa tarehe 22 Agosti mwaka 2014 . Hata hivyo halmashauri hiyo imesema inafurahia wajibu wanaotekeleza polisi katika kuzuia uhalifu na kudumisha utulivu. Imesema itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kuwafanya polisi kuwajibikia vitendo vyao.