Inter Milan Yamsajili Caner Erkin Kutoka Fenerbahce

Inter Milan imekamilisha usajili wa Caner Erkin kutoka katika kilabu cha Fenerbahce kwa kandarasi ya miaka mitatu.A� Kandarasi ya mlinzi huyo na kilabu hicho cha Uturuki itakamilika mwishoni mwa mwezi huu na miamba hao wa Italia wamethibitisha usajili wake.A� Caner, aliyejumwishwa na kocha Fatih Terim katika kikosi cha wachezaji 23 cha timu ya Uturuki kitakachoshiriki kwenye fainali za kombe la mataifa bingwa barani Ulaya atajiunga na timu yake mpya tarehe moja wezi Julai.