Inter Milan yakanusha madai ya kumsajili kocha wa Chelsea Antonio Conte

Inter Milan imekataa kuzungumzia habari kuwa kilabu hicho kinapania kumsajili kocha wa Chelsea Antonio Conte atakayechukua nafasi ya A�Stefano Pioli aliyefutwa kazi .Duru za kuaminika nchini Italia zimedokeza kuwa Inter Milan inayomilikiwa na kampuni ya Uchina iko tayari kumpa Conte mkataba wa pauni 250,000 kila juma ikiwa ataihama Chelsea kwa msimu mmoja. Pioli alifutwa kazi jumanne wiki hii, miezi sita baada ya kuteuliwa. Kocha huyo aliye na umri wa miaka 51 alichukua mahali pa Frank de Boer mwezi Novemba na kutia saini mkataba ambao ungetamatika mwezi juni mwaka 2018. Conte aliifunza timu ya taifa ya Italia na vilevileA� A�Juventus kati ya mwaka 2011-2014. Huku zikiwa zimesalia mechi tatu msimu ukamilike Inter inashikilia nafasi ya saba msururuni na haijaandikisha ushindi katika mechi saba za Serie A ambazo imecheza.