Inspecta Jenerali Awaonya Wanasiasa Kutoka Laikipia, Samburu Na Baringo Dhidi Ya Uchochezi

Inspekta jenerali wa Polisi Joseph Boinnet amewaonya wanasiasa na wanaharakati kutoka kaunty za Laikipia, Samburu na Baringo dhidi ya kuwachochea wachungaji wa Mifugo akisema watashtakiwa.Boinnet amesema uchunguzi umefichua kwamba wengi wa wanasiasa na wanaharakati wamekuwa wakichochea ongezeko la zisizo halali ikiwa ni pamoja na ulishaji mifugo katika mashamba ya kibinafsi bila idhidi katika kaunty ya Laikipia.Kwenye taarifa, inspekta generali amesema Oparesheni ya kuwakamata wahusika imeanzishwa na wale watakaopatikana na hatia watashtakiwa.Kulingana na taarifa hiyo, kamishna wa kaunty hiyo ameagizwa kumkamata mtu yeyote anayevurugha amani.Sehemu zilizoathiriwa ni pamoja na Muge, Laikipa Nature Conservancy, Shamba la ADC Mutara , Lampara na Gorare katika kaunty ya Laikipia.