Ingwe yailaza KCCA ya Uganda 2-1 katika mechi ya kirafiki

Timu inayoshiriki ligi kuuA� ya soka humu nchini AFC Leopards iliwashinda vigogo wa Uganda KCCA mabao 2-1 kwenye mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa katika uwanja wa Machakos. Mechi hiyo ilikuwa ya nne ya kirafiki A�kwa Leopards baada ya kuilemea Gatanga FC mabao kumi kwa sifuri, kisha ikaishinda Bidco United mabao mawili kwa sifuri na hatimaye kuilaza Thika United mabao mawili kwa moja. KCCA ilishindwa mabao manne kwa mawiliA� na A�Gor Mahia kabla ya kuishinda Tusker FC bao moja kwa sifuri katika uwanja wa Ruaraka. Timu zote mbili zinajiandaa kwa michuano yaA� bara Afrika na ligi za nyumbani. AFC Leopards itawakilisha Kenya kwenye kombe la mashirikisho barani Afrika ambapo itachuanaA� na Fosa Juniors kwenye mechi ya mwondoano huku A�KCCA ikikabiliana na CNAPS A�Sport ya Madagascar kwenye mechi ya mwondoano ya ligi ya mabingwa Barani Afrika.