IGAD Yapendekeza Kuondolewa Kwa Wanajeshi Watiifu Kwa Rais Wa Sudan Kusini, Salva Kiir

Shirika la IGAD limependekeza kuondolewa kwa wanajeshi watiifu kwa rais rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na makamu wake wa kwanza, Riek Machar mjini Juba na mahali pao pachukuliwe na kikosi cha walinda amani kutoka nchi za kanda hii. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uganda, Henry Okello Oryem amesema kikao cha IGAD kinachoendelea pembezoni mwa mkutano wa Jumuia ya Afrika mjini Kigali, Rwanda pia kimeunga mkono mapendekezo ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ya kukiimarisha kikosi cha wahifadhi amani wa Umoja huo nchini Sudan Kusini. Alisema swala muhimu ni kuhakikisha uthabiti wa mji wa Juba na sio tu kuangazia mzozo unaokumba Sudan Kusini.