IGAD yaelezea masikitiko yake kuhusu marudio ya uchaguzi

Shirika la IGAD limeelezea masikitiko yake kuhusu taarifa na vitendo vya baadhi ya wadau kuhusiana na marudio ya uchaguzi wa urais. Kwenye taarifa kwa vyumba vya habari, katibu mkuu wa IGAD balozi Mahboub Maalim alisema taarifa na vitendo vinavyofanya watu kutilia shaka uwezo wa tume ya IEBC kusimamia marudio ya uchaguzi wa Urais; Masharti magumu yanayotatiza matayarisho ya marudio ya uchaguzi;A� Na pia miito ya kususia uchaguziA� huo, vinaiweka nchi hii hatarini. Maalim alisema shirika hilo la IGAD lina imani kwamba tume ya IEBC ina uwezo wa kutekeleza jukumu lake la kikatiba; Nalo ni kusimamia uchaguzi. IGAD imesema hujuma zozote kwa tume ya IEBC, ama kususiwa kwa uchaguzi kutaiweka nchi hii kwenye mzozo wa kikatiba na kupelekea mabadiliko ya serikali kwa njia zisizo za ki-katiba. Shirika hilo sasa linahimiza wahusika wote kuwakataa wale wenye nia ya kuvuruga katiba kwa kutatiza au kuzuia marudio ya uchaguzi wa urais, kwa sababu hii inahatarisha mabadiliko ya kidemokrasia ya serikali.