IEBC yateua maafisa wapya kusimamia uchaguzi

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC, Wafula Chebukati, ambaye ndiye afisa wa kitafa wa kusimamia uchaguzi ameteuwa kundi la mradi wa kusimamia marudio ya uchaguzi wa urais tarehe 17 mwezi ujao. Mshirikishi wa mradi huo atakuwa Marjan Hussein ilhali mkuu wa oparesheni atakuwa Sidney Namulungu. Mkuu wa mipangilio ni Nancy Kariuki ilhali mkuu wa mafunzo ni Bernard Misati Moseti. Mkuu wa kituo cha taifa cha kujumlisha kura atakuwa Silas Rotich ilhali mkuu wa teknolojia ya habari na mawasiliano ni Albert Gogo chini ya usimamizi wa Chebukati. Uteuzi wao utadumu kwa muda wa miezi mitatu. Mwenyekiti huyo wa tume ya IEBC amesema imejitolea kuhakikisha uchauzi huo wa urais utazingatia kwa dhati katiba, sheria husika na utabainisha azma ya Wakenya.