IEBC yataka shilingi bilioni 3.7 zaidi – Chiloba

Afisa mkuu wa tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC Ezra Chiloba ameiambia kamati ya bunge inayoshughulikia bajeti ya ziada kwamba tume hiyo inahitaji shilingi bilioni 3.7 zaidiA� kwa marudio ya uchaguzi wa urais.Tayari tume hiyo imetengewa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya marudio ya uchaguzi huo. Chiloba alisema pesa hizo za ziada zitatumika kuimarisha mfumo uliotangamanishwa wa uchaguzi yaani KIEMS na kuwalipa zaidi ya makarani laki tatu wa uchaguzi ambao tume hiyo inanuia kuajiri .Mbunge wa Kipkelion mashariki Joseph Limo hata hivyo alisema watapendekeza nyongeza ya shilingi bilioni 2 pekee .Chiloba pia aliihakikishia tume hiyo vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya marudio ya uchaguzi huo vitakuwa tayari kwa wakati .