IEBC Yasikitishwa Na Idadi Ndogo Ya Wasajiliwa Wa Kura

Tume huru ya uchagazi na mipaka IEBC imeelezea masikitiko yake kufuatia idadi ndogo ya watu wanaojitokeza kusajiliwa kuwa wapiga kura huku shughuli hiyo ikiingia siku ya tano.IEBC imetoa wito kwa wakenya kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kuwa wapiga kura badala ya kusubiri mikimbio ya dakika za mwisho.Akiongea mjini Eldoret, Mshirikishi wa tume ya IEBC katika enoe la North Rift Bilha Kiptugen amesema idadi hiyo ingali ndogo mnoA� tangu shughuli hiyo ianze jumatatu wiki hii.Huko Kisumu , gavana wa kaunti hiyoA� Jack Ranguma ametangaza zawadi kwa wadi za kuanty hiyo zitakazowasajili wapiga kura wengi huku kaunti hiyo ikikusudiwa kuwasajili wapiga kura elfu 250 zaidi.Mkenya yeyote ambaye hakusajiliwa kuwa mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu uliopita au wale ambao wamepata vitambulisho vipya wanahimizwa kujitokeza wasajiliwe kabla ya uchgauzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka ujao.IEBC inalenga kuwasajili takriban wapiga kura milioni nne wapya kwenye shughuli inayoendelea ya kuwasajili wapiga kura.