IEBC yakutana kujadili uchaguzi ujao

Tume ya IEBC inakutana kwa mara ya kwanza tangu mahakama ya juu iagize marudio ya uchaguzi wa urais mnamo ijumaa wiki iliyopita. Ajenda kuu ya mkutano huo ni kutenga tarehe ya uchaguzi huo mpya ambao sharti uandaliwe katika muda wa siku 60 zijazo. Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula ChebukatiA� alikuwa amesema kwamba mkutano huo utapendekeza mabadiliko yatakayotekelezwa katika makao makuu ya tume hiyo huku ikijiandaa kwa marudio ya uchaguzi wa urais. Chebukati alimtaka mkurugenzi wa mashtaka ya umma kuchunguza na kumshtaki afisa yeyote wa tume hiyo ambaye huenda alikiuka sheria wakati wa uchaguzi mkuu mwezi jana. Chebukati alisema yeyote atakayepatikana alikiuka kanuni za uchaguzi na kusababisha kubatilishwa na matokeo ya uchaguzi wa urais lazima awajibike.