IEBC yafungua mitambo ya kupeperusha matokeo

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, Wafula Chebukati jana alisema kuwa tume hiyo ilifungua mitandao/mitambo yake ya kupeperusha matokeo ya uchaguzi wa urais kwa ukaguzi. Kwenye taarifa katika mtandao wake wa  twitter,  Chebukati alisema kuwa haki hiyo ilitolewa kutokana na ombi lililotolewa na wagombezi wa urais pamoja na maajenti wao na wachunguzi wakati wa marudio ya uchaguzi ya tarehe 26 mwezi huu ambapo rais Uhuru Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi hapo jana. Hatua ya tume hiyo ya kukosa kufungua  mitandao yake kukaguliwa baada ya kutangaza matokeo ndio baadhi ya sababu zilizochangia  kufutiliwa mbali kwa uchaguzi wa urais wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu baada ya upinzani kuwasilishwa kesi katika mahakama ya juu.