IEBC imeongeza siku mbili za usajili wa wapiga kura

Mahakama kuu imeiagiza tume huru ya uchaguzi na mipakaA� IEBC kuongeza kwa siku mbili muda wa usajili wa wapiga kura.Jaji Chacha Mwita alitoa agizo hilo kufwatia ombi lililowasilishwa na mwanaharakati Okiya Omtatah ambaye alidai kuwa shughuli hiyo inaweza tu kusimamishwa miezi miwili kabla ya uchaguzi.Kufwatia uamuzi huo wa mahakama,makamishna wa tume ya uchaguzi waliandaa kikao cha dharura kujadili gharama ya agizo hilo,ambalo hata hivyo wanasema wataheshimu baada ya kupokea rasmi agizo hilo. Habari zaidi zinasema mamia ya Wakenya walipanga foleni katika vituo mbali mbali vya usajili wa wapiga kura , kujisajili katika siku ya mwisho ya shughuli hiyo.Na huku hayo yakijiri,baadhi ya viongozi wa kisiasa wametoa wito wa kuongezwa kwa muda wa usajili wa wapiga,wakisema maelfu ya watu wangali wanasubiri vitambulisho.Kadhalika idadi kubwa ya wapiga kura wanaotaka kubadilisha vituo vya kupigia kura,walifika katika ofisi za tume ya uchaguzi katika maeneo bunge,ambapo walisailiwa kabla ya kuidhinishwa.Tume ya uchaguzi ililenga kuwasajili wapiga kura wapya million 6,lakini hadi sasa imefanikiwa kuwasajili wapiga kura wapya million 2.1.