IEBC Haitaongeza Muda Wa Usajili Wa Wapiga Kura

Tume huru ya uchaguzi na mipaka a��IEBC imesema kuwa haitaongeza muda wa usajili wa wapiga kura baada ya kukamilika kwa muda uliotangazwa.Naibu mwenyekiti wa tume hiyo Consolata Nkatha amesema shughuli hiyo itakamilika rasmi siku ya jumanne tarehe 14 mwezi huu. Akiongea katika sehemu ya Nchaure katika kaunti ndogo ya Imenti Kaskazini,kwenye kaunti ya Meru, Nkatha alisema alisimama katika vituo kadhaa vya usajili wa wapiga kura ,akiwa njiani kutoka Nairobi kuelekea Meru,na kusema ameridhishwa na idadi ya watu waliojitokeza kujisajili.Alisema tume hiyo ina ratiba yenye shughuli nyingi ya kusanifisha sajili ya wapiga kura kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao unaandaliwa kwa njia ya haki.

Aliwahimiza wale ambao hawajajisajili kutumia siku mbili zilizosalia kufanya hivyo ili tume hiyo iwe na wakati wa kutosha kukagua sajili ya wapiga kura. Na kuhusu usajili wa wafungwa walio na vitambulisho,alisema maandalizi yamekamilika na kwamba shughuli itachukua muda wa juma moja kukamilika .