Idadi Ya Wanaohamia Bara Ulaya Yazua Wasi Wasi

Idadi ya wahamiaji wanaoingia barani ulaya iliongezeka sana mnamo miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu,huku mataifa mengi katika bara hilo A�yakiimarisha ulinzi mipakani.Jambo hilo limezua hali ya wasi wasi miongoni mwa mashirika ya kutoa misaada na yale ya kutetea haki za binadamu.Siku ya jumanne shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia wakimbizi-UNHCR lilisema kuwa takriban wakimbizi 131,724 walivukaA� bahari ya Medittaranean mnamo miezi ya Januari na Februari,huku wengine 122,637 wakiingia Ugiriki.Takriban wakimbizi 418 walifariki dunia wakiwa njiani kuelekeaA� bara ulaya katika kipindi hicho,ikilinganishwa na wakimbizi 428 mwaka jana kulingana na shirika la kimataifa la kushughulikia wahamiaji-IOM.Shirika hilo linasema kuwa takriban wakimbiziA� 321, walikufa maji wakiwa njiani kuelekea Ugiriki,77 kati yao wakiwa watoto.Inakadiriwa kuwa mtoto A�mmoja hufariki dunia kila siku katika harakati za kutaka kuvuka bahari hiyo na kuingia bara ulaya.