Idadi ya waliofariki kutokana na kipindupindu nchini Zimbabwe yaongezeka

Idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu nchini Zimbabwe imeongezeka hadi watu 25. Hayo yamejiri huku shirika la afya duniani-WHO likionya kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka ,kwani ugonjwa huo unasambaa haraka katika mji mkuu wa nchi hiyo ,Harare.

Shirika hilo hata hivyo limesema limeimarisha juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo katika mji mkuu huo,ambao unakisiwa kuwa na zaidi ya wakazi million mbili.Tayari mikutano ya umma imepigwa marufuku mjini humo,huku maafisa wa wizara ya afya wakisimamia mazishi ya waliofariki kutokana ugonjwa huo.