Ibrahim Ghandour asema Sudan inashirikiana na Chad kuchunguza kisa cha utekaji nyara nchini Chad

Sudan inashirikiana na maafisa wa utawala nchini A�Chad na Ufaransa katika uchunguzi wa kisa ambapo raia mmoja wa Ufaransa alitekwa nyara nchini Chad na kupelekwa nchini A�A�Sudan. Haya ni kwa mujibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa taifa hilo Ibrahim Ghandour. Ghandour alisema kuwa Sudan inashirikiana na Chad kupitia vikosi vya pamoja vya kufanya uchunguzi. Hakukuwa na habari zozote za kundi lolote kudai kuhusika na utekaji nyara huo. Raia mmoja wa Ufaransa alitekwa nyara siku ya alhamisi kusini ya mji wa A�Abeche ambao huhusika zaidi na uchimbaji madini. Mji huo ni takriban kilomita 800 mashariki ya mji mkuu wa Chad A�A�N’Djamena na kilomita A�150 kutoka katika mpaka wa Sudan. Visa vya utekaji nyara huwa nadra sana nchini A�Chad na lakini eneo hilo la mashariki katika mpaka wa taifa hilo limekuwa likishuhudia visa kadhaa kutoka kwa makundi yaliyojihami wakiwemo waasi wanaopigana dhidi ya serikali ya Sudan.Sudan inashirikiana na maafisa wa utawala nchini A�Chad na Ufaransa katika uchunguzi wa kisa ambapo raia mmoja wa Ufaransa alitekwa nyara nchini Chad na kupelekwa nchini A�A�Sudan. Haya ni kwa mujibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa taifa hilo Ibrahim Ghandour. Ghandour alisema kuwa Sudan inashirikiana na Chad kupitia vikosi vya pamoja vya kufanya uchunguzi. Hakukuwa na habari zozote za kundi lolote kudai kuhusika na utekaji nyara huo. Raia mmoja wa Ufaransa alitekwa nyara siku ya alhamisi kusini ya mji wa A�Abeche ambao huhusika zaidi na uchimbaji madini. Mji huo ni takriban kilomita 800 mashariki ya mji mkuu wa Chad A�A�N’Djamena na kilomita A�150 kutoka katika mpaka wa Sudan. Visa vya utekaji nyara huwa nadra sana nchini A�Chad na lakini eneo hilo la mashariki katika mpaka wa taifa hilo limekuwa likishuhudia visa kadhaa kutoka kwa makundi yaliyojihami wakiwemo waasi wanaopigana dhidi ya serikali ya Sudan.