Ibada ya wafu ya wanafunzi 11 waandaliwa kesho

Dayosisi ya Kitui ya kanisa Katoliki siku ya Jumatano itaandaa ibada ya pamoja ya wafu kwa wanafunzi 11 wa shule ya mabweni ya St. Gabriel waliofariki kwenye ajali ya barabarani ambayo ilihusisha Lori na Basi la shule yao usiku wa Jumamosi. Kulingana na taarifa ya Rev. Joseph Mwongela, wa Dayosisi ya Kitui  kanisa hilo limeathirika vibaya na ajali hiyo na litaandaa ibada ya wafu siku ya Alhamisi katika kanisa la St. Josephs minor Seminary huko Mwingi. Aidha, kanisa katoliki linachangisha fedha za kuwaandalia wanafunzi hao mazishi ya heshima. Hayo yanajiri huku kundi moja la maafisa wa kukadria ubora wa viwango likiendelea kuchunguza chanzo haswa cha ajali hiyo kabla ya kuwasilisha ripoti ya mwisho kwa wizara ya elimu. Ripoti ya mwanzo hapo jana, inaashiria kwamba wakati wa ajali hiyo Bus hilo lilikuwa limewabeba wanafunzi 47, waalimu watatu na pia Matron wa shule hiyo . Wizara ya elimu imeziagiza shule zote kuzinghatia kikamilifu masharti yaliyoko kuhusu safari za wanafunzi hususan wiki hii ambapo tamasha la kitaifa la Muziki linaendelea huko Nyeri.