Hussein Dado na Halima Ware wajiunga na chama cha Jubilee

Gavana wa Tana River, Hussein Dado pamoja na mwakilishi wa wanawake katika kaunti hiyo, Halima Ware jana waliuhama upinzani na kujiunga na Jubilee. Wawili hao walikuwa wameteuliwa kupitia chama cha Wiper Democratic wakati wa uchaguzi mkuu uliopita. Walitangaza hayo jana walipouongoza ujumbe wa kukutana na rais katika ikulu ya Mombasa.A� Wakiandamana na seneta wa Tana River Ali Bule, viongozi hao walisema walijiunga na Jubilee kwa hiari. Akiwapokea katika ikulu ya Mombasa, rais Uhuru Kenyatta aliwashukuru kwa uamuzi huo wa busara na kusema amekuwa akitamani sana kushirikiana nao. Rais alisema serikali ya kitaifa imekuwa ikishirikiana kwa karibu na serikali ya kaunti ya Tana River kwa manufaa ya kaunti hiyo.