Hungary Victor Orban apata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu

Waziri mkuu anaegemea mrengo wa shoto nchini Hungary Viktor Orban amedai kupata ushindi mkubwa wakati wa uchaguzi mkuu wa siku ya Jumapili. Kiongozi huyo wa umri wa miaka 54 atahudumia kipindi cha tatu uongozini huku chama chake cha Fidesz kikibashiri kudumisha wingi wake wa uwakilishi wa thuluthi mbili bungeni . Chama hicho cha Fidesz kilijipatia takriban nusu ya kura asilimia 93 zilizohesabiwa kulingana na afisi ya kura za kitaifa nchini humo . Katika hotuba yake hapo jana jioni, Orban alisema kuwa ushindi wake utawapa raia wa nchi hiyo fursa ya kujitetea