Huduma ya polisi yatangaza nafasi za kazi

Tume ya huduma ya taifa ya polisi imetangaza nafasi tatu za ngazi za juu zilizo wazi katika huduma ya polisi. Nafasi hizo ni zile za naibu inspekta jenerali wa polisi wa kawaida, naibu inspekta jenerali wa polisi wa utawala na nafasi wa mkurugenzi wa idara ya upelelezi  wa jinai. Tangazo la tume hiyo inayoongozwa na Johnston Kavuludi linajiri baada ya rais kumuondoa Joel Kitili na kumteua  Edward Njoroge Mbugua kuwa kaimu naibu inspekta jenerali wa polisi wa kawaida na Noor Yarao Gabao kuwa kaimu naibu inspekta jenerali wa polisi wa utawala kuchukua mahala pa Samuel Arachi. Aliyekuwa msemaji wa polisi George Maingi Kinoti aliteuliwa kaimu mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai