Htin Kyaw Akaribia Kuwa Rais Wa Myanmar

Mmoja wa washirika wa karibu wa Aung San Suu Kyi alithibitishwa leo kwenye kuraya bunge kuwa mmoja wa wagombezi watatu wa Urais wa Myanmar.Htin Kyaw wa chama cha National League for Democracy aliithinishwa kwa kura 274-29 katika bunge la lower kuwa kwenye mkondo wa mwisho wa uteuzi wa mgombezi wa urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi wa wiki ijayo.Mgombezi wa pili wa chama hicho Henry Van Tio, alichaguliwa kuwa mgombezi wa pili na wa tatu atateuliwa na bunge ambalo limepewa asilimia 25 ya uwakilishi bungeni kulingana na katiba ya nchi hiyo.Wabunge kutoka mabunge yote mawili yatafanya duru nyingine ya upigaji kura ambayo tarehe yake bado haijatangazwa ambapo mmoja wa wagombezi hao atachaguliwa kuwa Rais.wengine wawili watakuwa makamu wa Rais.