Hospitali Ya Kenyatta Yapewa Mtambo Wa Saratani

Hospitali kuu ya Kenyatta imepokea mtambo wa kisasa wa kupima A�saratani ya matiti utakaoboresha uwezo wa taasisi hiyo kukabiliana na maradhi ya saratani. Mama wa taifa Margaret Kenyatta alinukuliwa wakati alipotoa mtambo huo kwa hospitali hiyo katika afisi yake. Pia ilikuwa siku ya kuzindua ushirikiano mpya kati ya kampuni ya dawa la Roche Pharmaceuticals na wizara ya afya kwa lengo la kuimarisha matibabu ya ugonjwa wa saratani ya matiti. Mama wa taifa alisema licha ya upungufu wa vifaa pamoja na wataalam, hospitali ya Kenyatta imekuwa ikiwashughulikia wagonjwa wa saratani wa humu nchini na hata kutoka mataifa mengine kwa muda mrefu. Mama Margaret alitoa wito kwa viongozi kuunga mkono mipango ya kuzuia na kutibu maradhi ya saratani.

Mtambo huo mpya ni watatu nchini na ndio mkubwa zaidi. Mitambo nyingine aina hiyo inamilikiwa na hospitali za Aga Khan, Nairobi, na mahabara za Lancet A�kwenye barabara ya A�Ngong.