Hospitali ya Kenyatta yakanusha madai ya kifo cha mgonjwa katika mchanganyiko wa upasuaji

Hospitali kuu ya Kenyatta imekanusha madai yalioripotiwa kupitia baadhi ya vyombo vya habari kuwa mmoja wa wagonjwa waliohusika katika mchanganyiko wa matibabu ya upasuaji amefariki. Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, hospitali hiyo imesema kuwa wagonjwa hao wawili bado wanaendelea kupata matibabu katika wadi na wanaendelea kupata nafuu. Wakati huo huo, viongozi kutoka eneo la Rift Valley wamemtetea afisa mkuu wa hospitali hiyo Lily Koros na kusema kuna juhudi kutoka kwa baadhi ya watu za kuwafurusha wataalamu kutoka jamii Fulani katika nyadhifa za uongozi na mahala pao kuchukuliwa na watu wanaopendekezwa na wale walioko katika ngazi za juu za uongozi . Wakiongozwa na gavawa wa Kericho Paul Chepkwony, viongozi hao walidai kuwa kesi ya madai yaA� ubakaji iliyoripotiwa katika hospiatli hiyo ilishughulikiwa vilivyo na afisi ya mkurugenzi wa mashatka ya umma na kamati ya bunge kuhusu afya ikaiondolea lawama hospitali hiyo .