Homa ya ndege aina ya H5N8 yaripotiwa Afrika kusini

Jimbo la Western Cape nchini Afrika kusini limeripoti visaA� ugonjwa wa homa ya ndege aina ya H5N8 kwenye mashamba mawili ya ufugaji wa mbuni. Kwenye taarifa idara ya kilimo ya jimbo hilo ilisema kuwa hatua madhubuti zimechukuliwa kukabiliana na maradhi hayo kwenye mashamba hayo mawili. Idara hiyo iliongeza kuwa hakuna vifo vya ndege vilivyoripotiwa katika sehemu hiyo na inashukiwa kuwa ndege za mwituni huenda ndizo zilisambaza ugonjwa huo. Idara hiyo ilisema kuwa kuna zaidi ya mbuni elf moja kwenye mashamba hayo mawili. Hatahivyo shirika la afya duniani WHO limesema hakuna uwezekano wa maradhi hayo kuambukiza binadamu.