Hatimaye Rais Akubali Mazungumzo Kufanyika

Rais Uhuru Kenyatta amekubali kuteua kundi litakaloshauriana na lile la Muungano wa CORD kuhusiana na suala la tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC. Kwenye hotuba yake kwa taifa hapo jana, Rais Kenyatta alisema kufuatia mashauriano na spika wa bunge la Senate na mwenzake wa bunge la Kitaifa na viongozi wa kidini katika ikulu ya Nairobi, wamekubaliana kubuni jopo kutoka mabunge yote mawili ambalo litatafuta suluhisho kwa mzozo wa tume ya IEBC. Alisema kulingana na kanuni za mabunge yote mawili, wadau wote, secta ya uma na ile ya kibinafsi wanafaa kupewa fursa ya kuwasilisha maoni yao kwa kamati hiyo ya pamoja.A�Rais ameitisha mkutano wa kundi la wabunge wa jubilee hivi elo asubuhi ili kukubaliana kuhusu ushiriki wa Jubilee kwenye kamati hiyo. Kwenye taarifa kwa vyumba vya habari , kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi amesema hatua hiyo ya Rais ni ishara ya heri njema na uongozi mzuri. Mudavadi alisema jopo hilo halipasi tu kuzingatia makamishna wa IEBC pekee bali pia marekebisho ambayo tume hiyo inafaa kufanyiwa.A�A� A�