Hatima Ya Wakimbizi Haijulikani Baada Ya Serikali Kuvunjilia Mbali Idara Ya Maswala Ya Wakimbizi

Serikali imesema kwamba mzigo mkubwa wa kifedha kwa Kenya ni mojawapo wa sababu zilizoifanya kuamua kuvunja idara ya maswala ya wakimbizi. A�Waziri wa fedha Henry Rotich hata hivyo amesema serikali inafanya mipango ya kushauriana na wadau wa kimataifa ili kusaidia kupatikana kwa suluhisho la kudumu kwa mzozo wa wakimbizi unaotokota huku Jumuiya ya Ulaya ikisema kwamba imetoa Euro millioni 200 kusaidia mpango wa kuwarejesha nchini mwao kwa hiari wakimbizi wa Somalia. Tangu siku ya ijumaa hatima ya zidi ya wakimbizi alfu-600 wanaoishi humu nchini haibainiki baada ya serikli kufunga idara ya maswala ya wakimbizi. Rotich alisema kwamba kwa muda wa miaka-30 Kenya imebeba mzigo wa kiuchumi ambao umesababishwa na ongezeko la wakimbizi humu nchini. Huku akikiri juhudi za Kenya katika kushughuliki mzozo wa wakimbizi katika eneo la Afrika mashariki afisa mkuu wa Ujumbe wa Jumuiya ya Ulaya humu nchini Balozi Stefano Dejak alisema mashauriano ya kina yatafanywa ili kusaidia kushughulikia maswala ambayo yamewasilishwa na Kenya. A�Mzozo wa wakimbizi umekuwa tatizo kubwa duniani huko nchi kama vile Uturuki zikitoa makataa kwa Jumuiya ya Ulaya endapo inataka nchi hiyo kuwapatia hifadhi wakimbizi wanaotoroka nchini Syria.