Hart Amuaga Mkufunzi Wake Wa Manchester City

Mlindalango wa Manchester City Joe Hart amesema wachezaji wa timu hiyo wanampenda Manuel Pellegrini na wanafurahia akiwa mkufunzi wao. Mzaliwa huyo wa Chile, ambaye timu yake ina uwezo wa kutwaa mataji 4 msimu huu, atanga��atuka wadhifani mwishoni mwa msimu naye Pep Guardiola achukue mahali pake. Tangazo hilo lilitolewa siku ya Jumatatu, saa 24 kabla ya City kuishinda Sunderland bao moja kwa bila. Ushindi huo, katika mchuano wa 100 wa Pallegrini mamlakani, uliiacha City alama tatu nyuma ya vinara Leicester katika orodha ya ligi kuu nchini Uingereza. Leicester itachuana na City Jumamosi hii uwanjani Etihad.