Harambee Stars Imepanda Safu Hadi Nafasi Ya 87

Timu ya taifa ya soka Harambee stars imepanda nafasi mbili katika orodha ya hivi punde ya timu bora duniani iliyotolewa jana.A� Timi hiyo ya taifa sasa inashikilia nafasi ya 87 duniani ilihali iko katika nafasi ya 20 barani Afrika.A� UgandaA� inayoshikilia nafasi ya 77 duniani bado ni timu bora katika eneo la Afrika masharikiA� ilihali RwandaA� inashikilia nafasi ya 93 duniani. EthiopiaA�A� iko katika nafasi ya 112A� ilihaliTanzaniaA� iko nyuma ya Kenya katika nafasi ya 88. Senegal ni ya kwanza barani Afrika na kufuatiwa na mabingwa watetezi wa kombe la bara Afrika Kodivaa.A� Misri, Tunisia, Algeria zinakamilisha orodha ya timu tano bora ilihali Ghana iliyofuzu kwa mechi ya fainali za kombe la bara Afrika mwaka 2015 inashikilia nafasi ya nane. Duniani, Argentina, bado inaongoza na kufuatiwa na Brazil, Ujerumani, ChileA� na Ubelhiji.A� Columbia, Ufaransa, Ureno, Uruguay na Uhispania zinakamilisha orodha ya kumi bora.