Harambee Stars kuchuana na Thailand

Timu ya taifa ya soka Harambee Stars inanuia kujinusuru itakapochuana na ThailandA� Jumapili hii, baada ya ushinde wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Iraq uwanjani Basra, jana usiku.

Iraq, iliyokuwa ikichezea nyumbani kwa mara ya pili tangu shirikisho la soka duniani kufutiliambaliA� marufuku ya kuandaa mechi za kimataifa kwa sababu ya mhemko wa kisiasa nchini humo, ilichukua uongozi wa mabao mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa Brwa Nouri na Ahmed Khalif. Michael Olunga aliifungia Harambee bao la kufutia machozi huku timu hiyo ikijiandaa kucheza na Thailand Jumapili hii.