Harambee Stars kuchuana na Burundi kwenye nusu fainali ya CECAFA

Timu ya taifa ya soka, Harambee Stars, imewasili jijini Kisumu leo asubuhi salama salmini, tayari kwa mchuano wao wa nusu fainali ya mashindano ya CECAFA dhidi ya Burundi kesho, katika uwanja wa michezo wa Moi katika jiji hilo lililoko kando ya ziwa.Mashindano hayo yalipumzishwa kwa muda wa siku mbili jana na leo, kabla ya kuchezwa kwa mechi hizo mbili za nusu fainali. Mabingwa Uganda watachuana na Zanzibari katika nusu fainali ya pili siku Ijumaa hii. A�Kenya iliongoka kudini a�?Aa�� kwa alama nane, moja mbele ya Zanzibari nayo Uganda ikaongoza kundi a�?Ba�� kwa alama tano, sawa na Burundi, lakini ina ubora wa mabao. A�Stars inanuia kutwaa ubingwa wa mashindano hayo inapojiandaa kuimarisha kikosi chake kilichoshindwa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia, lakini kilishiriki katika fainali za kombe la Bara Afrika mara ya mwisho mwaka 2004 nchini Tunisia, ilikoondolewa katika awamu ya makundi.