Harambee Stars iko tayari kumenyana na Burundi

Kocha wa timu ya soka ya taifa Harambee Stars, Paul Put, amesema kikosi hicho ki tayari kumenyana na Burundi leo alasiri katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kuwania kombe la CECAFA,uwanjani Moi jijini Kisumu,saa tisa alasiri.

Timu hizo mbili zimechuana mara kumi katika mashindano yote tangu mwaka 2000, nne kati yazo ni katika mashindano ya CECAFA. Kati ya hizo Kenya imeshinda mechi mbili,imeshidwa tatu na kutoka sare mara tano. Harambee Stars ilifuzu kwa nusu fainali hiyo baada ya kuishinda Tanzania Bara bao moja kwa bila Jumatatu iliyopita na kuongoza kundi a�?Aa�� kwa alama nane, moja mbele ya Zanzibari itakayochuana na mabingwa watetezi Uganda Cranes katika mechi ya pili ya nusu fainali kesho alasiri, jijini Kisumu. Uganda Cranes itakosa huduma za walinzi wawili wa kutegemewa, Dennis Awany na Isaac Muleme waliooneshwa kadi nyekundu walipotoka sare na Ethiopia bao moja kwa moja Jumapili iliyopta. Mechi ya fainali itachezwa Jumapili hii katika uwanja wa Gatuzi la Machakos. Mechi hiyo itatanguliwa na mchuano baina ya washinde wa mechi ya leo na ile ya kesho, mjini Machakos