Harambee Starlets kupambana Na Ethiopia Au Aljeria

Shirikisho la soka barani Afrika, CAFA� limethibitisha kujiondoa kwa timu ya akinadada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika mechi za kufuzu kwa fainali za kuwania kombe la akinadada barani Afrika.

Timu hiyo ya Kongo ilipangwa kuchuana na Harambee Starlets mwishoni mwa juma hili katika awamu ya mwanzo ya makala ya kumi ya fainali za kuwania kombe la akinadada barani Afrika. Shirikisho la CAF, kupitia kwa barua iliyotumwa na naibu wa mkurugenzi wa idara ya mashindano ShereenA�Arafa,A� ilithibitisha kuwa Kenya sasa imefuzu moja kwa moja kwa raundi ijayo ya mechi za kufuzu kwa fainali hizo zinazoandaliwa kila baada ya miaka miwili.

Timu hiyo ya Starlets sasa itapambana na mshindi wa mechi baina ya Ethiopia na Aljeria zitakazocheza mwishoni mwa juma hili nchini Aljeria.

Starlets hata hivyo itaendelea kufanya mazoezi na imeratibu mechi kadhaa za kirafiki katika jitihada za kujiboresha tayari kwa michuano ijayo.Timu hiyo imekuwa mazoezini katika uwanja wa Kasarani kwa zaidi ya juma moja