Harambee Starlets Kuchuana na Aljeria siku ya Ijumaa

Timu ya taifa ya soka ya akinadada Harambee Starlets iliondoka humu nchini jana usiku kabla ya mechi ya mkondo wa kwanza ya kufuzu kwa fainali za Bara Afrika dhidi ya wenyeji Algeria Ijumaa hii jijini Algiers. Kikosi hicho cha Starlets chini ya kocha David Ouma kilifanya mazoezi yake ya mwisho hapo jana katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani.

OumaA� amekitaja kikosi dhabiti kinachojumwisha mchezaji mwenye makao yake nchini Uganda Mary Kinuthia, Mwanahalima Adam, Wendy Achieng, Neddy Atieno na Dorcas Shikobe miongoni mwa wachezaji wengine. Timu hiyo ya taifa itakuwa ikinuia kuandikisha matokeo bora baada ya kubanduliwa na a�?Banyana Banyanaa�� ya Afrika Kusini katika raundi ya mwisho ya mechi za kufuzu kwa michezo ya Olimpiki.

Aidha, Kenya ilifuzu kuchuana na Algeria baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kujiondoa kwenye mechi hizo nayo Algeria ikailemea Ethiopia. Mashindano hayo ya Bara Afrika kwa akinadada yataandaliwa kati ya tarehe kumi na tisa mwezi Novemba na tarehe tatu mwezi Disemba nchini Cameroon.