Harambee Starlets Kuchuana Na Aljeria Katika Mechi Ya Kufuzu Kwa Kombe La Akina Dada Barani Afrika

Timu ya taifa ya soka kwa akina dada, Harambee Starlets itachuana na Algeria leo alasiri katika mechi ya marudiano ya kufuzu kwa fainali za kuwania kombe la akina dada barani Afrika uwanjani Moi Kasarani. Starlets itacheza mechi hiyo ikiongoza kwa mabao 2-0 ya ugenini baada ya kutoka sare kwa kufungana mabao 2-2 na Aljeria katika mechi ya mkondo wa kwanza. Warembo hao wa humu nchini wanahitaji sare ya 0-0 ao 1-1 ili kuboresha matumaini yao ya kufuzu kwa makala ya mwaka huu ya kombe la akina dada barani Afrika yatakayoandaliwa mwezi Disemba ambapo jumla ya timu 8 zitashiriki.A�A� Kocha mkuu wa Harambee Starlets David Ouma amewashirikisha wachezaji wengi walioshiriki katika mkondo wa kwanza. Nahodha Anne Aluoch ambaye alikosa mechi ya mkondo wa kwanza amejumuishwa kuchukua nafasi ya Elizabeth Ambogo ambaye alijeruhiwa katika wakati wa mechi ya mkondo wa kwanza jijini Algiers.