Halmashauri ya Madawa na Sumu Nchini kukabliana nawauzaji madawa bila leseni

Halmashauri ya Madawa  na Sumu Nchini imeanza kukabiliana na watu wasiohitimu na wale wanaouza madawa  bila leseni katika kaunti ya Mombasa.  Halmashauri hiyo  inasema  misako ya ghafla  inalenga kuhakikisha sheria kuhusiana na maswala ya afya inaheshimiwa kikamilifu. Julius Kaluai, ambaye ni mkaguzi mkuu wa madawa  katika halmashauri hiyo anasema wataalam 40 bandia wa madawa  walikamatwa kwenye msako dhidi ya maduka haramu ya  kuuza madawa katika siku mbili zilizopita. Hata hivyo, aliongeza kuwa idadi ya waliokamatwa mwaka huu ni ndogo ikilinganishwa na  mwaka uliopita ambapo watu 70 walitiwa nguvuni.  Kaluai alisema wengi wa waliokamatwa ni wahudumu ambao hawana leseni na utaalam wa maswala ya dawa.  Alisema maduka ambayo  hayajasajiliwa  yanahifadhi na kuuza madawa katika mazingira mabofu  yanayoathiri  ubora wake na kuyayafanya yasiweze kutibubu magonjwa.