Halmashauri Ya Kukusanya Ushuru Kuzindua Mhuri Mpya.

KRA1

Watumiaji vileo, tumbaku na vinywaji vingine vinavyouzwa dukani sasa wanaweza kuthibitisha uhalali wa bidhaa wanazonunua kwa kutumia rununu zao baada ya halmashauri ya kukusanya ushuru hapa nchini kuzindua mhuri mpya. Mhuri huo ulio na alama ya siri pia utawawezesha wauzaji bidhaa kuthibitisha uhalisi wa bidhaa wanazolipia ushuru.

Msimamizi wa idara ya ushuru wa humu nchini katika halmashauri ya KRA, Benson Korongo amesema mhuri huo mpya pia utaiwezesha halmashauri hiyo kuziba mianya ambayo imekuwa ikichangia kutoweka kwa mapato yake. Kupitia mfumo huo mpya, halmashauri ya kukusanya ushuru hapa nchini inanuia kuwekeza katika uthibitishaji wa bidhaa ili kupata asilimia-10 ya ukuaji wa mapato yake kwa mwaka. Hata hivyo mihuri ya awali iliyowekwa katika katika mivinyo, sigara na pombe ingali inatumika hadi bidhaa zote zilizokuwa zimepigwa mihuri hiyo zimalizike.A�A�