Halmashauri ya kitaifa yagawa vyakula na mifugo huko kajiado

Halmashauri ya kitaifa ya kukabiliana na mikasa leo imeanza kugawa vyakula vya mifugo kwa wafugaji huko Kajiado katika jitihada za kuwakinga mifugo wao kutokana na baa la njaa.A�Mpango huo unalenga kuwakinga wafugaji kutokana na hasara ya kuwapoteza mifugo yao kutokana na hali ya ukame katika eneo hilo.A�A�Serikali imegawa zaidi ya gunia elfuA�A�420 za nyasi na marobota elfu saba ya nyasi kwa zaidi ya wakulimaA�A�katika maeneo yaliyoathirika. Chakula hiki cha msaada kwa mifugo kinalenga maeneo manne ambayo yameathirika vibaya na hali ya ukame. Naibu gavana wa kaunti yaA�A�Kajiado Martin Moshisho amesema kuwa lishe hiyo ina virutubishi vya kutosha na itakuwa muhimu kwa mifugo huku wanaposubiriA�A�nyasi kumea. Maafisa wa kaunti wamepewa changamoto ya kuhakikisha kuwa chakula hicho cha msaada kinawafikia wote walioathirika. Wakati huo huo, wakazi wametahadharishwa kujiepusha na maeneo ya mabondeni na mito ya misimu wakati huu wa msimu wa kubwa zisizoweza kutabirika ili kuepuka vifo kama ambavyo imeshuhudiwa katika siku zilizopita.A�