Hali Ya Tahadhari Yatangazwa Nchini Ubelgiji Huku Polisi Wakiwasaka Wanagambo

Hali ya tahadhari imetangazwa  mjini Brussels ,huko Ubelgiji huku polisi wakiendeleza msako wao dhidi ya wanamgmbo wa kiislamu  waliotekeleza mashambulizi mjini Paris Ufaransa tarehe 13 mwezi wa Novemba mwaka jana.Washukiwa wawili wanadhaniwa wamejificha kwenye jumba moja viungani mwa  msitu mmoja ulio karibu na mji huo.Maafisa wanne wa polisi walijeruhiwa kwenye kisa hicho,huku mshukiwa aliyekuwa na bunduki aina ya Kalashnikov akiuawa  nje ya jumba moja.Operesheni hiyo inahusishwa na  mashambulizi yaliotekelezwa  mwaka jana mjini Paris na kusababisha vifo vya watu 130.Wanamgambo wa Islamic State walidai kutekeleza shambulizi hilo.Mshukiwa huyo aliyeuawa hata hivyo hakuwa mshukiwa mkuu Salah Abdeslam jinsi ilivyodhaniwa.