Hali ya kawaida yarejea katika makazi ya naibu rais William Ruto

Hali ya kawaida imerejea katika makazi ya naibu rais William Ruto huko Sugoi baada ya maafisa wa kitengo cha RecceA� kukabiliana na mshambulizi ambaye alikuwa amemteka nyara afisa wa polisi aliyekuwa kazini. Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett amesema afisa mmoja wa polisi alipoteza maisha yake wakati wa shambulizi hilo, ilhali mwingine alilazwa hospitalini. Boinett alisema makabiliano hayo yalikamilika leo asubuhi na mshambulizi huyo kuuawa. Uchunguzi unaendelea kumtambua mshambulizi huyo na waliko maafisa wengine wa ulinzi ambao walitarajiwa kuwa kazini. Na akiongea katika kaunti ya Muranga��a, Ruto alisema shambulizi hilo lilikuwa jaribio la kuibua hali ya taharuki miongoni mwa Wakenya kabla ya uchaguzi mkuu. Alisema hatayumbishwa na kisa hicho na akawahimiza Wakenya kujiepusha na wale wanaohujumu umoja na amani hapa nchini.