Hakutakuwa Na Maendeleo Iwapo Wanawake Watabaguliwa-Wabunge

Wabunge wanawake wamewalaumu wenzao wa kiume kwa kutatiza juhudiA� za kufikia sheria ya usawa wa kijinsia katika nyadhifa za kuchaguliwa . Wakiongozwa na Rose Nyamunga waA� Kisumu, Mishi MbokoA� wa Mombasa na Susan Musyoka waMachakos wabunge hao wanawake waliwashutumu wenzao wa kiume kwa kuupotosha umma kwamba mswada wa marekebisho ya katiba unapaswa kupitishwa kama ulivyo hivi sasa ili kuepusha kuvunjwa kwa bunge. Wakichangia mswada huo uliowasilishwa na mwenyekiti wa kamati ya bunge la taifa haki na sheriaA� Samuel Chepkonga ,wabunge hao wanawake walisema wametumia mbinu zote kutafuta kuungwa mkono na wenzao wa kiume kuafikia sheria hiyo bila mafanikio .

Wakipinga mswada huo wabunge Kibra Ken Okoth , Wesley Korir wa Cherangany na Opiyo Wandayi wa ugunja walisema hakutakuwa na maendeleo ya maana ikiwa wanawake watabaguliwa. Walisema uwakilishi wa kijinsia haupaswi kukomea bunge pekee.