Hakuna Muda Bainifu Wa ICC Kutangaza Uamuzi

Hakuna muda kamili uliotolewa kwa mahakama ya ICC kutangaza uamuzi wake kuhusu hoja iliyowasilishwa na mawakili wa Naibu wa Rais William Ruto na Joshua arap Sang kwamba hakuna kesi ya kujibu.

Mratibu wa ICC hapa nchini na nchini Uganda, Maria Kamara, amesema umauzi huo umo mikononi mwa majaji wa ICC ambao watatoa uamuzi huo hadharani.

Hata hivyo Kamara alikuwa haraka kuongeza kwamba uamuzi huo unaosubiriwa hauna uhusiano na matumizi ya ushahidi uliokanwa Kuhusu kibali cha kukamatwa kwa mwanahabari wa zamani Walter Baraza na wakenya wengine wawili kuhusiana na kuwatatiza mashahidi, Kamara amesema wanachukuliwa kuwa watoro.

Wakili wa waathiriwa wa Ghasia za baada ya uchaguzi Wilfred Nderitu alisema katika kesi hiyo kuwa uamuzi wa majaji kwamba hakuna kesi ya kujibu kwa kesi za wakenya waliosalia utakuwa pigo kwa waathiriwa ambao wanahitaji kuwa haki itatekelezwa. mashahidi 29 wametoa ushahidi wao dhidi ya Ruto na Sang tangu kesi hiyo ilipoanza hapo mwaka wa 2013, huku mashahidi 5 wakiondoa ushahidi wao