Human Rights Watch Yakosoa Misri Kuhusu Haki Za Kibinadamu

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema katika ripoti yake iliyotolewa jana kuwa utawala nchini Misri umepiga maarufuku ukosoaji wa hadharani na upinzani nchini humo. Ripoti hiyo inadai kuwa vikosi vya usalama huwatesa wafungwa huku mamia ya wafungwa wakiripotiwa kutoweka mwaka uliopita. A�Katika ripoti yake kwa jina “World Report 2017,” shirika hilo lenye makao yake jijini A�New York lilisema kuwa serikali ya rais A�Abdel-Fattah el-Sisi imechukua hatua isiyo ya kawaida ya kuharamisha shughuli za mashirika ya kutetea haki za binadamu na kulemaza mashirika ya kijamii. El-Sisi aliongoza mapinduzi ya kijeshi ya mwaka wa 2013 ambayo yalimwondoa mamlakani rais wa kwanza kuchaguliwa kwa huru na haki nchini humo Mohammed Morsi. Rais huyo ameongoza misako mbalimbali ambayo imesababisha kukamatwa kwa maelfu ya watu wengi wao wakiwa wafuasi wa Morsi na baadhi ya wanaharakati mashuhuri nchini humo.