Guatemala yamfukuza afisa wa umoja wa mataifa

Rais wa Guatemala amemfukuza mkuu wa kitengo cha ufisadi wa Umoja  wa mataifa kutoka nchini humo. Rais Jimmy Morales ameamuru Ivan Velasques Gomez kuondoka mara moja kutoka nchini humo,Kwenye ujumbe rasmi uliowekwa kwenye kanda. Japo mahakama ya nchi hiyo  ilisitisha utekelezaji wa agizo hilo mara moja, rais Morales alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kusitisha maamuzi yake kuhusu sera za kigeni. Shirika hilo limekuwa likiunga mkono  kufutiliwa mbali kwa kinga ya  kisiasa ya kiongozi huyo. Viongozi wa mashtaka nchini Guatemala wamemshutumu Rais Morales kwa  kugharimia visa vya ufisadi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Kwenye ujumbe wa video uliopachikwa  kwenye mtandao wa kijamii rais Morales alimtangaza Ivan Velasques ambaye ni rais wa Colombia na mwanasheria kitaaluma kuwa mtu asiyetakikana nchini humo.